Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, katika siku ya tatu tangia kufariki Sayyid Abdulkarim Nasrallah, baba mtukufu wa Bwana wa Mashahidi wa Umma, shahidi mtukufu Sayyid Hassan Nasrallah, Hizbullah iliandaa hafla ya kumbukumbu ndani ya Majma‘ Imam Mujtaba (amani iwe juu yake) huko Dhahiya ya Kusini ya Beirut.
Hafla hiyo ilihudhuriwa kwa wingi na shakhsia za kisiasa, vyama, kidiplomasia, kielimu, kidini na kijamii, pamoja na wabunge wa sasa na wa zamani na wawakilishi wa makundi ya Wapalestina nchini Lebanon.
Hafla ilianza kwa kusomwa aya kadhaa za Qur’ani Tukufu, kisha ikaendelea kwa hotuba ya Sheikh Naim Qassem, Katibu Mkuu wa Hizbullah. Katika hotuba yake alizungumzia maisha, mwenendo na watoto wema wa marehemu huyo, na kusisitiza kwamba marehemu alikuwa baba wa shakhsia mashuhuri na ya kipekee, Sayyid Hassan Nasrallah.
Katika mazungumzo na tovuti ya habari ya Al-Ahed, Mustafa Hamdan, Katibu wa Baraza la Uongozi wa “Harakati Huru ya N'asiriyun – Al-Murabitun”, alisema kuhusu marehemu Sayyid Abdulkarim Nasrallah: Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya roho ya baba wa Bwana wa Mashahidi wa Umma.
Aliongeza kuwa: Katika siku hizi ngumu, tumeelewa neno moja tu, nalo ni “Hayhata minna adh-dhillah” (uwe mbali nasi udhalili). Leo hatuna njia nyingine isipokuwa kusimama imara na kufanya mapambano dhidi ya njama zinazopangwa dhidi ya taifa letu na umma wetu.
Vilevile, kundi la wanazuoni wa Kipalestina waliokuja kutoa pole walisisitiza kuwa wajibu wa kidini, kimaadili, kibinadamu na kitaifa unawalazimu kushiriki katika hafla ya baba wa Bwana wa Mashahidi wa Umma; mtu aliyetoa maisha yake katika njia ya kadhia ya Palestina na ambaye naye mwenyewe alikufa shahidi katika njia ya Quds.
Walisisitiza kwamba; muqawama utaendelea kuwa chaguo la watu huru wa umma huu, hasa katika wakati ambao maadui wanapanga njama mbaya dhidi ya eneo hili na watu wake.
Maoni yako